Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora Revocatus Kuuli.

Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Kuuli leo tarehe 28 Desemba, 2020 kutokana na kukabiliwa na tuhuma za kujitwalia ardhi ya wananchi bila kufuata utaratibu, utendaji kazi usioridhisha na matumizi mabaya ya fedha za maduhuli ya Serikali.

Aidha, Rais Magufuli amemuagiza Mkuu wa Tabora Dkt. Phillemon Sengati kuteua Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo mara moja.

Chama abembelezwa kusaini mkataba mpya Simba SC
Kifaru: Tuna kikosi imara msimu huu

Comments

comments