Aliyekuwa nahodha wa Ndanda FC, Kigi Makasi amevua beji ya unahodha wa timu hiyo na kutimkia rasmi katika klabu ya Singida United.

Winga huyo aliyewahi kuitumikia timu ya Taifa (Taifa Stars) na Simba SC amekuwa mchezaji aliyefunga pazia la usajili katika klabu ya Singida United kwa msimu wa mwaka 2017/18, kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari.

Klabu ya Singida United imesajili wachezaji wapya 16 kwa ajili ya msimu huu mpya baada ya klabu hiyo kupanda daraja na kuwa miongoni mwa timu zinazominyana kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Kati ya wachezaji hao, wachezaji saba ni kutoka nchi za nje na wachezaji tisa kutoka ndani ya nchi. Timu hiyo ina jumla ya wachezaji 25 ikiwa ni pamoja na wachezaji tisa walioipandisha daraja.

Hii ni orodha ya wachezaji saba kutoka nje ya nchi:

1.Elisha Muroiwa(Zimbabwe)

2.Twafadzwa Kutinyu (Zimbabwe)

3.Simbarashe Nhivi (Zimbabwe)

4.Wisdom Mtasa (Zimbabwe)

5.Shafik Batambuze(Uganda)

6.Dany Usengimana( Rwanda)

7.Michel Rusheshangoga(Rwanda)

Hii ni orodha ya wachezaji waliosajiliwa kutoka ndani ya nchi:

1.Atupele Green (Jk Ruvu)

2.Miraj Adam (Africa Lyion)

3.Kenny Ally (Mbeya City)

4.Roland Msonjo(Mshikamano FC)

5.Pastory Athans (Simba)

7.Deus Kaseke(Yanga)

8.Ally Mustapha (Yanga)

9.Kigi Makasi (Ndanda Fc).

Magazeti ya Tanzania leo Julai 24, 2017
Majaliwa amtumbua DED wa mbozi kwa matumizi mabaya ya fedha za umma