Rais wa Jamhuri ya muunga wa Tanzania Dkt John pombe Magufuli amesema Tanzania itajenga mtambo mkubwa wa kuchenjua madini ya niko kwa kushirikiana na Burundi.
Akizungumza katika uwanja wa Lake Tanganyika mkoani kigoma amesema ujenzi huo wa mtambo ni wamuhimu ili kuendelea kukuza mahusiano ya kiabishara na burundi pamoja na kukuza ajira kupitia ujenzi huo.
Mazungumzo yameshaanza lakini tunataka tuyafanye kwa haraka zaidi ili tuweze kujenga mtambo mkubwa na kuanza kuchenjua madini ya niko tuuze tupate fedha nyingi za kigeni na watu wetu wapate ajira”. Amesema Magufuli.
Aidha Rais Magufuli amesema kigoma itakuwa kituo cha biashara, ameongeza kuwa katika maongezi na raisi wa Burundi mengine watakayozungumzia ni pamoja na kuimarisha uwekezaji wa biashara, ujenzi wa reli kutoka uvinza, kisongati hadi kitega.
Amesema kuwa wataimarisha uhusiano wa wa biashara ya madini kwa kuruhusu burundi kuuuza madini yao katika soko la madini mkoani kigoma.