Jaji wa Mahakama ya Juu ya Marekani Ruth Bader Ginsburg, mpiganiaji wa haki za wanawake ambaye alikuwa jaji wa pili mwanamake katika mahakama hiyo, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 87

Kifo chake ambacho kimetokea wiki sita tu kabla ya Uchaguzi wa Rais huenda kikaanzisha mapambano makali ya kisiasa kuhusu kama Rais Donald Trump anapaswa kumteuwa mrithi wa Ruth na baraza la Seneti linalodhibitiwa na Warepublican liidhinishe au kubaki wazi mpaka uchaguzi.

Kiongozi wa Maseneta wa Republican Mitch McConnell amesema Seneti itapiga kura ya kuidhinisha au kupinga jaji atakayependekezwa na Trump kumrithi Ginsburg, hata ingawa ni mwaka wa uchaguzi. 

Aidha Trump amemuita Ruth “mwanamke wa ajabu” na hakutaja kuhusu kujaza kiti chake kilichobaki wazi katika Mahakama ya Juu, Naye Biden mgombea wa Republican amesema mshindi wa uchaguzi wa Novemba anapaswa kumchagua mrithi wa Ruth.

Kigoma kuwa kituo cha biashara ya madini
Bomba lenye uwezo wa kuonesha hali ya joto la maji