Mwili wa kijana mwenye miaka 17 aliyefahamika kwa jina la Devis Ayubu umeopolewa na jeshi la zimamoto na uokoaji baada ya kuzama ziwa Victoria wakati alipokuwa akiogelea na marafiki zake.

Akizungumza baada ya zoezi la uopoaji maeneo ya fukwe za ziwa Victoria, Kamishina msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Uokoaji Mkoa wa Kagera, SACP Zabrone Muhumhma amesema kijana huyo aliyeopolewa ni mkazi wa maeneo ya Hamgembe na alikuja kuogelea na rafiki yake ziwani hapo.

Amesema, “baada ya kupata taarifa Askari wamefika hapa kwenye eneo la tukio na kuweza kuopoa mwili wa kijana aliyezama na kukabidhiwa kwa jeshi la Polisi kwa taratibu zingine za kupelekwa hospitalini.”

Miongoni mwa mashuhuda waliokuwepo eneo hilo, Godian Gosbert akisimulia tukio amesema “nilimuuliza kwamba unamuona mwenzio anaomba msaada kule akanijibu yule anajua kuogelea vizuri tu, mara yule akanyosha mikono na kuzama jumla na sisi tukasema twende tukaite msaada Polisi.”

Maji ya Ziwa Victoria

Derick Ayubu ambaye ni ndugu wa Devis Ayubu ameeleza kuwa ndugu yake alimpigia simu akiwa nyumbani na kuja kuogelea ufukweni hapo ambapo yeye alikuwa akiogelea maeneo ya karibu na alipoona tukio hilo alikimbia kutoa taarifa kituo cha polisi kwa ajili ya kupata msaada.

Amesema, “mimi nilikuwa naogelea hapa karibu yeye na wenzake walikuwa mbali wanaogelea baadae wanakuja kuniambia mtu mwingine haonekani kuja kuangalia nikakuta mwenzangu ameshazama ikanibidi niende kituo cha polisi kutoa taarifa.”

Mwili huu ulio opolewa unafanya idadi ya watu walipoteza maisha wakati wakiogelea ndani ya fukwe za ziwa Victoria mjini Bukoba kufikiwa wawili.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Julai 11, 2023
Miaka 60 JKT yafana Rais Samia akitoa maelekezo