Jeshi la Sudan, Kikosi cha RSF kimesema kimefanikiwa kumuhamisha Rais wa zamani wa nchi hiyo, Omar al Bashir pamoja na maafisa wasiopungua watano wa utawala wake, kutoka katika Gereza la Kober na kuwapeleka Hospitali ya Jeshi.

Hatua hiyo inakuwa ni tukio la pili baada ya lile la wishoni mwa wiki iliyopita ambapo maelfu ya wafungwa waliachiwa kutoka gerezani, akiwemo waziri wa zamani katika Serikali ya Bashir, ambaye anatakiwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC, kwa makosa ya uhalifu wa kivita.

Hata hivyo, baadhi ya watu wamekuwa wakilaumu makundi yanayomtii Bashir kwa kutumia mzozo huo kutaka kumrejesha madarakani, huku wengi wao wakiwa wamekata tamaa na wakishindwa kutoka majumbani mwao kutokana na mapigano.

Kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa yanasema mapigano hayo, yamesabisha vifo vya watu wasiopungua 459 na majeruhi zaidi ya 4,000 huku Shirika la afya – WHO, likisema linataraji vifo kuongezeka hata zaidi kutokana na miripuko ya magonjwa na ukosefu wa huduma muhimu.

Kampuni za Simu mnaishi kwa kuwa Watanzania wana Afya - Nape
Zoezi ufukuaji miili waliofariki kwa mfungo tata lasitishwa