Chuo Kikuu Huria nchini kimemtunuku shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa ya mahusiano ya kimataifa, Rais wa serikali ya awamu ya nne, Dk. Jakaya Kikwete katika mahafali ya 30 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Chuo hicho kimemtunuku Dk. Kikwete shahada hiyo kutokana na mchango wake kwa jamii katika masuala ya kimataifa.

Shahada Kikwete

Baada ya kutunukiwa shahada hiyo na Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Dk. Asha Rose Migiro, rais huyo mstaafu alitoa shukurani zake kwa chuo hicho kwa kuona na kuthamini mchango wake.

“Naipokea heshima hii toka Chuo Kikuu Huria Tanzania kwa moyo mmoja kwani wameona mchango ambao nimeutoa nilipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Awamu ya Nne hivyo basi nitaendeleza mahusiano na ushirikiano kimataifa”.Alisema Dk.  Kikwete.

Bafetimbi Gomis Kurejeshwa Nyumbani Na PSG
Javier Mascherano Ahukumiwa Kwenda Jela