Uongozi wa Azam FC, umefikia makubaliano ya kumwongeza mkataba wa mwaka mmoja kiungo mkabaji raia wa Cameroon, Stephan Kingue ambaye alijiunga na klabu hiyo mwezi Novemba mwaka jana.

Akithibitisha nyongeza hiyo ya mkataba mbele ya waandishi wa habari leo mchana, Afisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd, amesema kuwa wamefikia uamuzi huo kufuatia mapendekezo ya Kocha mkuu, Aristica Cioaba ambaye anataka kuendelea na huduma yake.

“Uongozi wa juu wa Azam FC ulikuwa na mazungumzo na mchezaji Stephan Kingue Mpondo, amekuwa na timu kwa kipindi cha mwaka mmoja hivi sasa mkataba wake umekwisha na mazungumzo yalikuwa juzi na jana, lakini tunashukuru Mungu ni kwamba Stephan Mpondo kwa mujibu wa taarifa ya mwalimu Cioaba bado anamuhitaji kikosini”. Amesema Jaffar Idd.

Tanzania yaanguka nafasi sita viwango vya soka duniani

Kozi ya Grassroots yapelekwa Mbeya

Jaffar amesema Kingue ni mchezaji ambaye mwalimu amemkubali kwa maana ni mchezaji kiongozi uwanjani na moja ya sifa yake ni nidhamu na kujituma zaidi uwanjani.

Robson de Souza atupwa jela miaka tisa
Ndalichako ashikilia kidete ujenzi nyumba za walimu