Diwani wa Kata ya Mahohe kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Mohamed Ngonde amefariki akiwa katika ibada Msikitini.
Akithibitisha kifo hicho, Katibu wa Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Busoro Pazi amesema Marehemu Ngonde alifariki alfajiri leo Julai 8, 2022.
Pazi amesema taratibu za mazishi zitatolewa baada ya kukaa na familia ya marehemu.
“Kwa Sasa tunafanya taratibu za kwenda kuifadhi mwili wa marehemu katika hospitali ya Rufaa Mkoa Amana na taratibu za mazishi zitatolewa baada ya kukaa na familia ya marehemu,” amesema.
Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Wilaya ya Ilala Said Sidde amesema taarifa za Kifo cha Diwani huyo amezipata kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM kata Majohe ambapo amesema Marehemu Ngonde alifariki ghafla.
Naye Katibu Mwenezi wa CHama cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala, Alhaj Said Sidde amesema taarifa kamili zitatolewa kuhusiana na msiba huo.