Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo, imekubaliana kusogeza mbele matengenezo ya Uwanja wa Benjamin Mkapa ili kuipisha Young Africans kuutumia uwanja huo endapo itafanikiwa kutinga Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Young Africans inatarajia kucheza mchezo wa mkondo wa pili wa nusu fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Marumo Gallants, kweshokutwa Jumatano (Mei 17) nchini Afrika Kusini, ikiwa na mtaji wa mabao 2-0 ilioupata nyumbani.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Saidi Yakubu, amesema walipanga kuufunga uwanja huo mapema mwezi huu, lakini wameamua kusogeza mbele matengenezo hayo kwa kipindi cha mwezi mmoja zaidi baada ya kukubaliana na CAF kutokana mafanikio ya Young Africans kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.