Kiongozi Mkuu wa Upinzani nchini Uganda, kutoka chama cha Forum for Democratic Change FDC, Kizza Besigye amekamatwa na jeshi la polisi nchini humo kwa tuhuma za kutishia kuua.
Besigye amekamatwa katika kijiji cha Burimba, tarafa ya Bubare, Rubanda alipokuwa njiani kuelekea wilaya ya Kabale akitokea Rukungiri.
Kamanda wa Polisi wa mkoa, Denis Namuwoza amesema kuwa Besigye alikuwa anasakwa Rukungiri ambako anadaiwa alitenda makosa kadhaa ya kihalifu siku ya jumatano, likiwemo la kutishia kuua.
Amesema kuwa kosa jingine linalomkabili Besigye ni lile la kuruhusu wafuasi wake wa chama cha (FDC) kuwarushia mawe maafisa wa polisi ambao walikwenda kuwatawanya katika mkutano wa mwanasiasa huyo.
“Tunamshikilia kwa sababu anatafutwa, Rukungiri kwa kosa la kutishia kumuua afisa mmoja wa polisi na kuandaa mkutano haramu ambao hajapewa kibali, kwa hiyo amefanya kinyume na sheria,”amesema Namuwoza
-
Afisa wa tume ya uchaguzi Kenya IEBC ajiengua
-
Raila ateta na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi
-
Kenyatta apuuza wito wa Odinga
Hata hivyo, Besigye anashikiliwa na polisi pamoja wanasiasa wenzie ambao ni Patrick Amuriat na katibu wa uhamasishaji wa chama hicho Ingrid Turinawe.