Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Makamu wake William Ruto wamesema hawatafanya mazungumo na upinzani na wamesema kuwa wapo tayari uchaguzi ufanyike tarehe 26 Oktoba, 2017.

Hata hivyo amewaonya wanaopanga kufanya vurugu kuwashambulia maafisa wa tume na wapiga kura na kusema watadhibitiwa vikali na vyombo vya usalama.

Wakiongea katika mikutano katika Kaunti za Trans Zoia, Baringo na Laikipia, viongozi hao wa Jubilee wamepuuzia wito wa Raila Odinga kujadili mabadiliko katika tume ya uchaguzi kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio.

”Mazungumzo pekee nitakayofanya nitafanya na Wakenya, wapiga kura ambao nitaomba wanichague. Tume ya Uchaguzi imepewa Ksh. bilioni 12 kwa ajili ya kuendesha uchaguzi na sio kufanya mazungumzo na yoyote” amesema Uhuru Kenyatta.

Ameongezea pia ”Nimesikia wanataka kufanya mazungumzo na mimi. Sina muda na mazungumzo hayo, kama Raila hataki uchaguzi anaweza enda nyumbani na kulala na kuwaacha Wakenya watumie haki yao ya kikatiba

Video: Mwigamba abwaga manyanga ACT- Wazalendo
Messi afunga bao la 100 Barcelona ikiilaza Olympiakos