Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (KKKT) limejipanga kuendelea na zoezi la uuzaji wa viwanja vinavyomilikiwa na Kanisa hilo mkoani Njombe kutokana na maagizo ya kusitishwa uuzaji wa maeneo hayo lilitolewa na waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi alipokuwa mkoani Njombe siku chache zilizopita
Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kusini Njombe, Isaya Japhet Mengele amesema kuwa serikali kupitia wizara ya ardhi nyumba na makazi imeruhusu zoezi la uuzaji viwanja katika eneo linalojengwa chuo kikuu mjini Njombe baada ya kukamilisha maagizo yaliyotolewa na waziri, Wiliam Lukuvi ya kupata kibari kutoka kwa kamishina wa ardhi kanda ya nyanda za juu kusini.
Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake askofu Mengele amesema kuwa wamepokea barua kutoka wizara ya ardhi kupitia kwa mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa njombe ya kuendelea na uuzaji wa viwanja.
“Tumeruhusiwa kuendelea na zoezi la uuzaji wa viwanja katika eneo hilo la Lunyanywi ambalo lilikuwa limesimama kutokana na mgogoro uliokuwepo baina ya uongozi wa Dayosisi na baadhi ya waumini ambao kwa sasa umemalizika kufuatia maelekezo ya waziri wa Ardhi”amesema Askofu Mengele
-
Video: Walimu wabovu waziponza shule za Umma
-
Video: Gwajima ampongeza JPM, ‘Leo umekuwa Nabii’
-
Video: Makonda amchongea Tundu Lissu kwa JPM, ‘Akirudi apelekwe Milembe’
Hata hivyo, kusimamishwa kwa uuzwaji wa viwanja katika eneo la lunyanyu la ekari 1200 linalomilikiwa na chuo cha amani mjini Njombe kulitokana na mvutano uliojitokeza baina ya wadhamini wa bodi wa Kanisa hilo na baadhi ya waumini waliopinga mchakato huo kuendelea.