Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Karangwe , Benson Bagonza ametangaza kusitisha Ibada na mikusanyiko yote ya Dayosisi hiyo kuanzia Aprili 26, 2020 mpaka pale utaratibu mwingine utakapo tangazwa jimboni hapo.
Askofu Bagonza ametoa tamko hilo mara baada ya maambukizi ya ndani ya ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona kuzidi kuongezeka, Pia amewataka viongozi wengine wa dini kuiga mfano huo bila kusibiri serikali kuwatangazia.
Aidha Askofu Bagonza amesema shughuli za ibada na mikusanyiko yote jimboni humo itasitishwa lakini huduma za sakramenti zitatewa kwa makundi maalum tu kama wazee, Wagonjwa mahututi, mazishi na wale wanaotaka kubatizwa tu.
Ikumbukwe Serikali ya Tanzania imetangaza kuwa vingozi wa dini waendele na utoaji wa huduma lakini kwa tahadhari ya hali ya juu kwa kuweka maji, sabuni na dawa kuua vijidudu ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo.