Liverpool na Manchester United zinakutana Jumamosi hii katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza utakaopigwa katika dimba la Anfield wakati makocha wa timu hizo Jose Morinho na Jurgen wakitarajia kukutana kwa mara ya 8.
Jurgen Klopp anaamini Liverpool itashinda kutokana na rekodi nzuri mbele ya Mourinho kwani katika michezo 7 waliyokutana Klopp ameshinda mara 3 Mourinho akishinda mara moja tu huku wakisuluhu mara 3.
Tangu mwaka 2014 Liverpool walipoipiga Manchester United bao 3 kwa 0, klabu hiyo haijawahi kupata ushindi tena dhidi ya Man Utd kwenye mechi zilizofuata, safari hii United wanakwenda Anfield wakiwa wanajiamini kwani katika michezo mitano iliyopita waliyocheza hapo United wameshinda mara 3 wakipata suluhu 1 na kupoteza mara 1.
Kama Liverpool wakipoteza mchezo huu itakuwa habari mbaya kwa Klopp kwani mwaka 2014 Brenden Rodgers alifukuzwa baada ya kupata alama 12 katika mechi 8 sawa na ambazo Klopp atazipata kama akipoteza mchezo huu.
Manchester United wanaoonekana kutaka kuendeleza wimbi la ushindi wanaweza kuweka rekodi mpya ya kufikisha alama 22 katika michezo 8 ya Epl kama wakiibuka na ushindi dhidi ya Liverpool.
Manchester United watawakosa Paul Pogba na Maroane Fellaini huku ngome yao ya ulinzi ikiwapa jeuri kubwa ambapo kwa mwaka huu tu 2017 hawajaruhusu goli ktika michezo 17 idadi ambayo hakuna klabu waliyoifikia.
Mchezo huo hautakuwa na urahisi kwa pande zote kwani Liverpool pamoja na kumkosa Sadio Mane lakini wanao Mohamed Salah na Coutinho.