Benchi la Ufundi wa Ihefu FC limesisitiza kupambana vilivyo katika michezo ya lala salama ya Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kuangusha alama tatu mbele ya Simba SC, kwa kufungwa 2-0 kwenye Uwanja wa nyumbani wa Highland Estate.

Kabla ya mchezo huo, mara ya mwisho Ihefu kupoteza katika Uwanja wa nyumbani ilikuwa Novemba ll, 2022 ilipolala kwa mabao l-2 dhidi ya Polisi Tanzania kwa mabao ya Vitalis Mayanga na Samwel Onditi, wakati bao la Ihefu ikifungwa na Andrew Simchimba.

Kocha Msaidizi wa Ihefu, Zuber Katwila, amesema wanafahamu wanachokifanya na wala hilo haliwapi presha japo wanatakiwa kuwa na tahadhari kubwa katika michezo ya kuelekea ukingoni mwa Ligi Kuu msimu huu.

“Tumeliona hilo mapema ndio maana hata mchezo uliopita dhidi ya Simba SC, nilisema namna matokeo yalivyotuathiri kwa kupoteza, lakini ndio mchezo ulivyo.”

“Tuna michezo iliyosalia nyumbani na ugenini, hivyo kama tutafanikiwa kupata matokeo mazuri katika michezo mitatu basi itakuwa imetusaidia sana,” amesema Katwila.

Ihefu kwa sasa inashika nafasi ya saba katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 33, huku wapinzani wake wa karibu ni Kagera na Mtibwa Sugar ambao wamepishana alama chache.

Imesalia michezo minne ambayo inaweza kubadilisha upepo kwa kila timu kama itafanya vibaya kwenye michezo hiyo na kujikuta eneo la hatari zaidi.

Timu mbili kutoka Mbeya, Tanzania Prisons na Mbeya City zote zimekaa kwenye hali ya presha kutokana na mwenendo mbovu wao hasa mzunguko wa pili wa ligi.

Ihefu kwa mara ya kwanza ilipanda Ligi Kuu msimu wa 2020/2 1l, haikudumu, ikashuka, kabla ya kurejea tena msimu huu wa 2022/23.

David de Gea kuongeza mwingine Man Utd
Tamko la Jeshi la Polisi kuelekea siku kuu ya Eid el-fitri