Nahodha na Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Senegal Sadio Mane atafanyia vipimo leo Jumatano (Novemba 09), ili kufahamu kama atakuwa sehemu ya kikosi kitakachoelekea Qatar kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia 2022.
Mane alipatwa na majeraha ya mguu jana Jumanne (Novemba 08) wakati wa mchezo wa Ligi ya Ujerumani ambapo Mabingwa watetezi FC Bayern Munich walikua nyumbani Allianz Arena wakicheza dhidi ya Werder Bremen.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30, alipatwa na jeraha la mguu dakika ya 15 ya mchezo huo uliomalizika kwa Bayern Munich kushinda mabao 6-1, na nafasi yake kuchukuliwa na Leroy Sane.
Meneja wa FC Bayern Munich Julian Nagelsmann amesema Mane alipatwa na majeraha ya mguu kwa kugonga sehemu ya mfupa wa Tibia. Hivyo alilazimika kutoka nje kutokana na kuhisi maumivu makali.
Amesema Mane atafanyiwa vipimo vya X-ray leo Jumatano (Novemba 09), hivyo anatarajia majibu yatakuwa mazuri na atajiunga na wenzake kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia zitakazoanza kurindima baadae mwezi huu.
Mshambuliaji huyo amepatwa na jeraha hilo, zikisalia siku 13 kabla ya mchezo wa kwanza kwa Senegal ambapo itapapatuana na Uholanzi kwenye Fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar.
Katika Fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar, Senegal imepangwa Kundi A sambamba na timu za taifa za Ecuador, Uholanzi na Wenyeji Qatar.
Mane anashikilia Rekodi ya kuwa Mshambuliaji wa Senegal aliyefunga mabao mengi zaidi, akifunga mabao 34, huku akikumbukwa kwa mkwaju wake wa Penati iliyoipa Taji la Afrika taifa hilo la Afrika Magharibi, mapema mwaka huu dhidi ya Misri.
Mane anaungana na wachezaji wengine wa Senegal ambao wapo kwenye hatihati ya kushiriki Fainali za Kombe la Dunia 2022 kutokana na majeraha yanayowakabili katika kipindi hiki.
Wachezaji hao ni Edouard Mendy na Kalidou Koulibaly wanaoitumikia Klabu ya Chelsea pamoja na Idrissa Gueye wa Klabu ya Everton.
Jana Jumanne (Novemba 08), Kocha Mkuu wa Senegal Aliou Cisse alitangaza kikosi cha wachezaji 26 kwa ajili ya Fainali hizo.
Walinda Lango: Alfred Gomis (Rennes), Seny Dieng (QPR) na Mory Diaw (Clermont).
Mabeki: Kalidou Koulibaly (Chelsea), Pape Abou Cisse (Olympiacos), Fode Ballo-Toure (AC Milan), Noah Fadiga (Brest), Ismail Jakobs (Monaco), Formose Mendy (Amiens), Moussa Niakhate (Nottingham Forest) na Abdou Diallo (RB Leipzig)
Viungo: Idrissa Gueye (Everton), Pathe Ciss (Rayo Vallecano), Cheikhou Kouyate (Nottingham Forest), Pape Gueye (Marseille), Krepin Diatta (Monaco), Nampalys Mendy (Leicester), Pape Matar Sarr (Tottenham), Mamadou Loum (Reading) na Moustapha Name (Pafos).
Washambuliaji: Sadio Mane (Bayern Munich), Boulaye Dia (Salernitana), Bamba Dieng (Marseille), Ismaila Sarr (Watford), Iliman Ndiaye (Sheffield United), Nicolas Jackson (Villarreal), Demba Seck (Torino) na Habib Diallo (Strasbourg)
Wachezaji ambao wameitwa na kuweka kwenye orodha mbadala Walinda Lango: Edouard Mendy (Chelsea), Alioune Badara Faty (Casa Sports) na Bingourou Kamara (Montpellier)
Mabeki: Noah Fadiga (Brest), Saliou Ciss, Youssouf Sabaly (Real Betis), Abdoulaye Seck (Maccabi Haifa), Alpha Diounkou (Barcelona B), Bouna Sarr (Bayern Munich) na Ibrahima Mbaye (CFR Cluj)
Viungo: Joseph Lopy (Sochaux) na Boubakary Soumare (Leicester City)