Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amekosoa wafadhili wa kimataifa kwa kufanya kuwa vigumu kwa mataifa maskini kupata misaada ya kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Akizungumza katika mkutano wa kilele wa COP27 siku ya Jumanne, Rais Ramaphosa aliomba kuwekwa wazi kwa suala hilo huku mamlaka za usalama zikilazimika kumsindikiza mbunge anayeiunga mkono serikali ya Misri Amri Darwish baada ya kuvuruga mkutano wa waandishi wa habari ulioongozwa na dada wa mwanaharakati aliyefungwa jela kutoka Uingereza na Misri ambaye kwa sasa amegoma kula.

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa.

Mwanaharakati huyo ambaye kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka mitano, alishtakiwa kwa kueneza taarifa potofu baada ya kukashifu ukatili wa Polisi kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa ripoti inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa iliyotolewa Novemba 7, 2022, imesema nchi zinazoendelea na nchi zinazoinukia kiuchumi, zinahitaji uwekezaji wa zaidi ya dola trilioni 2 kila mwaka ifikapo 2030.

Gazeti la L'Equipe lachafua hali ya hewa
Kombe la Dunia 2022: Sadio Mane azua hofu Senegal