Kaimu Mtendaji wa Latra CCC, Leo Ngowi amesema kuwa, Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini limekata mapendekezo ya nauli yaliyotolewa na wadau wa usafiri wa masafa marefu na mafupi.
Ngowi amesema kuwa safari za mjini ni fupi na abiria wengi wamekuwa wakipanda na kushuka njiani huku mabasi hayo kubeba abiria kupita kiasi.
Uwamuzi huo umefikiwa leo Jumatano Aprili 13, 2022 baada ya Umoja wa Wasafirishaji Abiria Mkoa wa Dar es Salaam kupendekeza kiwango cha nauli kuwa mara mbili ya nauli inayotozwa sasa.
“Tunapendekeza wasilisho hili lirudishwe kwa mtoa huduma, lakini kama wanazungumzia hasara pia tunashauri kutumia mfumo wa kuzuia mianya ya upotevu kwa kumtumia tiketi mtandao,” amesema Ngowi.
Akiwasilisha viwango hivyo Katibu wa umoja huo, Suleiman Kimwe amesema umependekeza viwango vya nauli kuwa mara mbili ya ilivyo sasa
“Kwa maoni yetu tunaomba ongezeko la nauli ya Sh400 kwa kila njia. Mfano kwa nauli ya Sh500 iwe Sh900 “amesema Kimwe.