Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema kuwa yeye hawezi kupigana na Meya wa Ubungo, Boniface Jacob kwa masuala ya siasa.
Ameyasema hayo mara baada ya kutoka katika kikao cha kamati kuu ya chama hicho kilichokuwa kinatathmini uchaguzi mdogo wa madiwani uliopita.
Amesema kuwa kuna tetesi nyingi kuhusu utabiri alioutoa kuhusu mwanachama mwenzie na mbunge Kibamba, John Mnyika kuhusu kuhama chama hicho.
“Hapo majuzi nilitoa utabiri wangu, na nikasema kuwa kuna baadhi ya wabunge wa Chadema watakihama chama chetu, kwa sasa siwezi sema chochote baada ya kikao hiki cha kamati kuu, tusubiri mwenyekiti ndio atakayetoa mstakabari wa kinachoendelea,”amesema Lema
Hata hivyo, ameongeza kuwa hana ugomvi wowote na mbunge wa jimbo la Kibamba, John Mnyika kama taarifa zilijvyoenea katika miyandao ya kijamii.
-
Zitto: Viongozi wengi wa kisiasa ni wanafiki
-
Video: Lissu awanyooshea kidole Bunge & Polisi, Kumekucha CCM