Mbunge wa Arusha Mjini, Gobless Lema amewaomba Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchema na IGP Sirro kuwaachia watu waliokamatwa jana na jeshi la polisi wakiwa wamevaa Tshirt za Tundu Lissu na Ukuta.
Ameyasema hayo kupitia mitandao yake ya kijamii na kudai kuwa watu ambao wameratibu maombi kwa ajili ya Lissu hawakupaswa kukamatwa bali walipaswa kulindwa na jeshi la polisi.
”Mwigulu Nchemba wewe ni Waziri wa Mambo ya Ndani na IGP Sirro tunakuomba sana waachie watu wote waliokamatwa wakiwa wamevaa Tshirt za UKUTA waachie kwa sababu walichokuwa wanakifanya ni kitu kizuri hawakuwa na nia mbaya,” ameandika Lema.
Hata hivyo, Lema ametoa kauli hiyo siku moja baada ya jeshi la polisi kuzuia watu kufanya maombi ya kitaifa kwaajili ya Mbunge Tundu Lissu maombi ambayo yaliandaliwa na vijana wa CHADEMA (BAVICHA) ambayo yalipaswa kufanyika Septemba 17, 2017 katika viwanja vya TIP Sinza Darajani
-
Mbunge wa CCM aliyemkodia ndege Lissu atoboa siri
-
Wazee wa Kigoma wamjia juu Spika Ndugai
-
BAVICHA walibipu jeshi la polisi, wasema maombi yako palepale