Wabunge wao, wamewasilisha ushahidi huo mchana wa leo Oktoba 2, 2017 kwenye ofisi za Takukuru zilizopo Upanga Dar es Salaam, ambapo waliwasili kwa miguu na kuelekea moja kwa moja ndani.

Wameuwasilisha ushahidi huo ikiwa imepita siku moja tangu Lema na Nassari walipofanya mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha, kueleza jinsi madiwani wao walivyoshawishiwa kwa rushwa kuhama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Katika ushahidi huo walidai kuwa madiwani wao 10 waliohama Chadema walirubuniwa kwa rushwa, hivyo katika ushahidi wao walionyesha kuwa viongozi kadhaa wamerekodiwa wakiwashawishi madiwani hao kuhama na baadhi waliahidiwa wangelipwa posho za vikao vyao vilivyobaki hadi 2020 na kukamilishwa  miradi  yao.

Aidha, jana Jumapili Oktoba 1, 2017, Nassari ambaye akiwa ameambatana na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless  Lema walitoa ushahidi huo kwa waandishi wa habari na kueleza wataukabidhi Takukuru na katika taasisi nyingine.

Wakati Nassari akifanya hivyo tayari baadhi ya madiwani waliojiuzulu walisema kuwa hawakushawishiwa na mtu yeyote wala kupewa rushwa bali wamehama kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli.


Video: Kijiji alichotokea SHAABAN ROBERT: Familia yasimulia maisha yake, yadai kutonufaika na chochote

Hugo Broos: Ninafanya kazi bila mkataba
Timu ya taifa ya ngumi yaanza vizuri dhidi ya ngome