Beki wa kati kutoka nchini England, Joelon Lescott aliuwahi muda wa usajili wa majira ya kiangazia mbao ulifungwa rasmi jana jioni, kwa kujiunga na klabu ya Aston Villa akitokea West Bromwich Albion.

Lescot ametimkia Villa Park kwa ada ya uhamisho wa paund million mbili ambayo ilikubaliwa na viongozi wa klabu ya West Bromwich Albion, baada ya kuikataa ofa ya paund million moja hapo awali.

Lescott, mwenye umri wa miaka 33, alijiunga na klabu ya West Brom akiwa mchezaji huru baada ya kumalizana na Man City na kuondoka kwake The Hawthorns kumepewa baraka zote na meneja Tony Pulis.

Lescott ambaye alifanikiwa kutwaa ubingwa wa nchini England mara mbili, kombe la FA pamoja na kombe la ligi mara moja akiwa na klabu ya Man City, kwa kipindi kirefu alikua shabiki mkubwa wa klabu ya Aston Villa na kuelekea huko katika maisha ya soka lake kutamtimizia lengo alilokua akilikusudia tangu akiwa na umri wa miaka 17.

Kukamilishwa kwa usajili huo siku ya mwisho, kulimpa ujasiri meneja wa Aston Villa, Tim Sherwood ambaye alionekana kuzungumza na kwenye televisheni ya klabu hiyo kwa kujiamini wakati wote.

Sherwood, alisema ni hatua nzuri aliyoifanikisha kumsajili beki huyo, na sasa anaamini kikosi chake kimepata nguvu mpya katika safu ya ulinzi.

Kabla ya kusajiliwa kwa Lescott, Aston Villa walikua wanahusishwa na mpango wa kutaka kumsajili beki wa klabu ya Liverpool, Tiago Ilori ambaye dakika za mwisho alielekea Crystal Palace.

Los Angeles Kuwania Nafasi 2024
Gwajima Amjibu Dk. Slaa