Mtangazaji wa vipindi vya The Switch na Big Sunday vya Wasafi FM/TV, Omary Tambwe maarufu kama Lil Ommy, ametajwa kwa mwaka wa pili mfululizo kuwania Tuzo za African Entertainment Awards (AEAUSA) zinazotolewa Marekani, kama Mtangazaji Bora Afrika.

Oktoba 2019, Lil Ommy aliibuka mshindi kwenye tuzo hizo, hivyo hadi sasa ndiye anayeshikilia nafasi hiyo inayowaniwa tena, kama Mtangazaji Bora Afrika, akiiwakilisha vyema Tanzania.

Lil Ommy ameiambia Dar24 Media kuwa kwakuwa yeye ndiye Mtangazaji pekee wa Tanzania anayewania tuzo hiyo, anawaomba Watanzania wote wampigie kura ili Tanzania ishinde. Pia, amewashukuru tena kwa kumpa ushindi mwaka jana, akieleza kuwa “Tanzania ilishinda”.

Katika hatua nyingine, DJ Sinyorita wa Clouds FM, amechaguliwa kwa mara ya kwanza kuwania Tuzo ya DJ Bora Afrika katika tuzo hizo. Ni DJ wa kike na mtanzania pekee anayewania tuzo kwenye kipengele hiki.

Clouds wanaendelea kung’ara kwenye kipengele hiki, mwaka 2016 DJ D Ommy wa Clouds FM alishinda tuzo hii na kuwa DJ Bora Afrika; na miaka iliyofuatwa alitajwa kwenye kipengele hiki. Mwaka huu kituo hicho kimeng’ara tena na DJ mrembo.

Lil Ommy na DJ Sinyorita, ni Watanzania ambao wanawania tuzo hizi bila kuwa wanamuziki, wakiwakilisha kiwanda cha burudani kama wachezea santuri na utangazaji.

Kuwapigia kura bofya hapa https://bit.ly/33yI4Ve   Kisha chagua namba 24 (BEST HOST), bofya picha ya Lil Ommy, na DJ Sinyorita chagua namba 9 (BEST DJ) weka email yako na nchi unayotoka, kisha wasilisha. Tanzania inashinda.

Kwa upande wa wanamuziki, Diamond Patinumz ametajwa kwenye vipengele vingi ikiwa ni pamoja na Best Male Artist (Msanii Bora wa Kiume), Video Bora ya Muziki (Jeje)- na pia yeye na Harmonize wametajwa na wimbo wao ‘Kainama’ wakiwa na Burna Boy. Pia, Wimbo Bora wa Kushirikiana (Yope Remix) akiwa na Innoss’ B (Hapa wanapambana na Beyonce pia akiwa na wimbo wake ‘King Already’ aliomshirikisha Shatta.

Diamond, Harmonize na Ray Vanny wanakutana kwenye kipengele cha ‘Entertainment of the Year’. Zuchu naye amepenya kwenye kundi la Msanii Bora Mpya (Best New Artist)

Nandy na Maua Sama wamekutana pia kwenye kipengele cha ‘BEST FEMALE ARTIST – EAST/SOUTH/NORTH AFRICA’, huku Nandy akipenya pia kwenye kipengele cha ‘Best Female Artist’.

Ali Kiba amekutana na Harmonize, Diamond na Ray Vanny wanawania ‘Msanii Bora wa Mashariki/Kusini/Kaskazini mwa Afrika (BEST MALE ARTIST – EAST/SOUTH/NORTH AFRICA).

Tuzo hizi zitatolewa rasmi Desemba 12, 2020, Newark, New Jersey, MAREKANI.

Wapigie kura Watanzania, Tanzania inashinda.

Traore aitema Mali, aikubali Hispania
PSG yamnasa Rafinha dakika za mwisho