Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amemshauri Rais John Magufuli kuifumua Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2015/16 kwa madai kuwa haitekelezeki.

Profesa Lipumba ambaye amebobea katika masuala ya Uchumi amemshauri Rais Magufuli kutumia Bunge la Januari kuifanyia marekebisho bajeti hiyo ili iendane na mipango na ahadi zake.

“Ni wazi bajeti ambayo Rais Magufuli anairidhi ni bajeti ambayo haitekelezeki. Kwa hiyo ana wajibu wa kuandaa upya Bajeti na kwamba katika Bunge la Januari aweze kupelekea Mini-Budget itakayoleta marekebisho kuona kwamba mwaka huu wa fedha mambo yatatekelezwa namna gani,” alisema Profesa Lipumba.

“Kwa sababu unaweza kuwa umetamka tu umefuta ada, lakini ukakuta watoto wakienda shule hawajifunzi hadi waende ‘tuition’,” aliongeza.

Kadhalika, Profesa Lipumba alimtaka Rais Magufuli kuingilia kati mgogoro wa uchaguzi wa Zanzibar na kuiagiza Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Zanzibar kutangaza matokeo ya uchaguzi kwani wananchi wa Zanzibar walishamaliza uchaguzi na hawatakubali vinginevyo.

Alisema kuwa kwa kuwa yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu, ana uwezo mkubwa zaidi wa kufanya maamuzi juu ya suala hilo.

Wimbo Wa Taifa Wa Ufaransa Kusikika England
CUF waandamana jijini London, Zanzibar washangaa uteuzi wa Waziri Mkuu