Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amekiri kuwa ana deni kubwa na nchi ya Kenya kutokana na kuokoa maisha yake na kumpatia ulinzi kwa kipindi cha miezi minne aliyokuwepo nchini humo akitibiwa.
Ameyasema hayo mapema hii leo wakati akijiandaa kuondoka kuelekea nchini Ubelgiji anakoenda kwa ajili ya kufanya mazoezi ya viungo vya mwili ili aweze kutembea.
Amesema kuwa hataweza kusahau fadhila za nchi ya Kenya pamoja na watu wake kwani, serikali hiyo ilihakikisha inampatia ulinzi wa kutosha kwa masaa 24 alipokuwa hospitali hapo.
“Nina deni kubwa sana na nchi ya Kenya. Wakenya wameokoa maisha yangu na kunilinda kwa wakati wote. Ninashukrani kubwa kwa serikali ya Kenya na wananchi kwani madaktari wao na wauguzi wao wamehakikisha nakuwa hivi,”amesema Lissu
-
Mashinji ataja sababu za viongozi kuhama Chadema
-
Polepole atishia kung’oa kigogo wa Chadema
-
Video: Lissu adai alishambuliwa kisiasa
Hata hivyo, amewashukuru madaktari wa Dodoma kwa kuokoa maisha yake baada ya shambulio na kipekee amemshukuru Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Dkt. Mpoki Ulisubisya kwa kuwa Kiongozi mkuu wa jopo la madaktari waliookoa maisha yake na watanzania kwa maombi na michango yao.