Chama cha Mapinduzi CCM kimewateua kuwania nafasi za ubunge, wabunge waliojiuzulu upinzani na kuhamia katika chama hicho.

Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole imesema kuwa baada ya kufanyika kwa tathmini ya kina, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) imemteua Dkt. Godwin Mollel kugombea katika jimbo la SIHA, mkoani Kilimanjaro.

Aidha, Mgombea mwingine aliyeteuliwa ni Abdallah Mtulia ambaye atagombea Jimbo la Kinondoni lililopo jijini Dar es salaam.

Hata hivyo, taarifa hiyo imeelekezwa kufika katika ofisi za CCM mikoa husika ili waweze kupokea maelekezo husika yanayoihusu uchaguzi kutoka kwa makatibu wa CCM katika mikoa hiyo.

 

Mawaziri wawili wakamatwa kwa rushwa
Lissu awaachia ujumbe mzito Wakenya