Ikiwa ni siku ya mwisho ya dirisha la usajili nchini Uingereza klabu ya Liverpool imekamilisha usajili wa kiungo wa kati Alex Oxlade-Chamberlain kutoka katika klabu ya Arsenal kwa kiasi cha pauni milioni 35.

Chamberlain mwenye umri wa miaka 24 awali alikuwa akiwindwa na mabigwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza Chelsea lakini alikataa uhamisho huo siku ya Jumanne na sasa amejiunga na Liverpool kwa mkataba wa miaka mitano ambapo atakuwa akipokea £120,000 kwa wiki.

Kiungo huyo wa kati ameichezea klabu ya Arsenal mara 198 tangu ajiunge nayo kutoka katika klabu ya Southampton mnamo mwezi Agosti mwaka 2011 na amefanikiwa kuifungia timu hiyo jumla ya mabao 20.

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa anafurahi kumsajili mchezaji huyo mwenye uwezo mkubwa. Kocha hoyo ameongeza kuwa Chamberlain hakufanya maamuzi mepesi kuhama kutoka katika klabu kubwa lakini pia amefanya maamuzi maamuzi mazuri kwani amejiunga na klabu kubwa pia yenye vijana wenye vipaji.

Oxlade-Chamberlain akisaini mkataba

Tayari klabu ya Liverpool imemsajili winga Mohammed Salah kutoka Roma kwa pauni milioni 34, beki Andrew Robertson kutoka Hull City kwa pauni milioni 8 na mshambuliaji Dominic Solanke.

 

 

 

 

Arda Turan kutumika kama chambo kwa Mesut Ozil
Fenerbahce, Juventus zamuwania Marouane Fellaini