Muda mfupi baada ya taasisi ya Twaweza kutoa matokeo ya utafiti ulioonesha kuwa Mgombea Urais kupitia CCM, Dk John Magufuli anaongoza kwa 65% dhidi ya mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa, mgombea huyo amejibu mapigo akiwa jukwaani.

Akiongea katika mkutano wa kampeni mkoani Mtwara mbele ya maelfu ya wakazi wa eneo hilo, Edward Lowassa amewataka wananchi kutodanganyika na utafiti huo bali waujibu kwa mafuriko ya kura ifikapo Oktoba 25 mwaka huu.

“Sisi tujipange tuwajibu kwenye kura, nangoja kwa hamu mafuriko ya kura, tarehe 25 Oktoba mnipe kura,” alisema Lowassa.

Lowassa aliwaeleza wananchi hao kuhakikisha wanampigia kura na kwamba wanaweza kumtambua kwa haraka kwa kuangalia nywele zake zenye mvi kwani ndiye mgombea pekee mwenye nywele nyeupe (mvi) kichwa kizima.

Umati ukimsikiliza Lowassa Mtwara

Wakazi wa Mtwara wakimsikiliza Edward Lowassa

Katika hatua nyingine, viongozi wa Ukawa wawataka wananchi kuukataa utafiti huo kwa madai kuwa haukidhi vigezo kwa kuwahoji watu 1848 kuwakilisha watanzania milioni 24 waliojiandikisha kupiga kura.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliuita utafiti huo wa Twaweza kuwa ni utafiti usiozingatia taaluma (utafiti wa kikanjanja).

Hawa Ndio Wana Hip Hop Walioingiza Fedha Nyingi Zaidi Mwaka Huu ‘Cash Kings’
Navas Afichua Siri Nzito Iliyomkabili Siku Ya Mwisho