Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William lukuvi amewataka wananchi kuwa makini dhidi ya matapeli wa nyaraka za viwanja ambazo zimekuwa zikighushiwa kwaajili ya kuwadhurumu wananchi.
Ametoa tahadhari hiyo mapema hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akiendelea na zoezi la kutatua kero za viwanja kwa wananchi ambapo leo alikuwa akisikiliza na kuzitafutia ufumbuzi kero za wananchi wa wilaya ya Ilala.
“Wananchi nawaomba muwe makini sana, kuna matapeli wa ardhi siku hizi ambao wamekuwa wakighushi barua za toleo/ Offer Letter za wananchi, kwa hiyo ni bora mkachukua tahadhari mapema,”amesema Lukuvi.
Lukuvi amesema kuwa imebainika kuwa kuna Matapeli ambao wamekuwa wakishirikiana na maafisa ardhi ambao sio waaminifu na wamekuwa wakitumia barua za toleo za wananchi wa kipato cha chini kwa kutengeneza barua za toleo nyingine kwa viwanja ambavyo vimeshakwisha milikishwa.
-
Video: Jeshi la Polisi Rukwa lakamata vito vya thamani vilivyopitishwa kimagendo
-
Rais Magufuli awapandisha vyeo na kuwateua maafisa wawili wa zimamoto
-
Serikali yaongeza masaa ya mama kunyonyesha
Hata hivyo, Wananchi waliohudumiwa mapema hii leo wamepongeza hatua anazochukua Waziri Lukuvi katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili kwani wamekuwa wakiteseka kwa muda mrefu.