Kocha mkuu wa mabingwa wa soka Tanzania bara Young Africans, George Lwandamina, “Chicken” amesema kuwa kambi yao inaendelea vizuri kuelekea mchezo wa marejeano wa ligi ya mabingwa Afrika, dhidi ya wenyeji wao Township Rollers ya Botswana

Young Africans , ambayo imepiga kambi katika Hotel ya Crystal Palace mjini Gaborone, inataraji kutelemka dimbani siku ya Jumamosi kuwavaa Township mchezo utakaopigwa kunako uwanja wa taifa wa nchi hiyo

Akizungumza kutoka Botswana Lwandamina amesema kuwa wanaendelea vizuri na maandalizi yao na kikosi chake kipo vizuri, na wachezaji wana hari ya mchezo.

“Tunaendelea vizuri na maandalizi yetu, soka la Afrika kwa kiasi flani lipo sawa  kuanzia maeneo na hata vifaa vya mazoezi vinavyotumika” alisema Lwandamina

Kocha huyokutoka nchini Zambia aliweka wazi kuwa soka ni mchezo wa nguvu hivyo hataraji kwenye kikosi chake kutokuwa na mchezaji mwenye maumivu.

 

“Soka ni mchezo unaotumia nguvu hivyo siwezi kusema timu kutokuwa na mchezaji mwenye maumivu kabisa ” aliongeza kocha huyo asiye na maneno mengi

Young Africans  inahitaji ushindi wa mabao 2-0 ili kusonga mbele kwenye hatua ya makundi, baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 wakiwa nyumbani Jumanne ya wiki iliyopita

 

Michael Richard Wambura atupwa jela maisha
Simba SC wabisha hodi Port Said Misri