Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amewaagiza Ma- DC kuhakikisha wanapokwenda kuhamasisha kilimo kwa wananchi wawape hesabu namna watakavyonufaika.
Majaliwa amesema hayo leo Juni 13, 2021 katika mkutano wa kampeni ya kitaifa ya alizeti unliofanyika mkoani Singida.
Majaliwa amewataka wakuu wa wilaya kuacha kutoa maelezo ya jumla katika kilimo kwa wakulima na badala yake wawaeleze gharama zitakazotumika kwenye kilimo na faida atakayopata.
Aidha Waziri Mkuu amewataka wenye mabenki kutoa mikopo kwa wakulima ili kuwawezesha kupata mitaji na kulima kilimo chenye tija.
Katika hatua nyingine Wakuu wa Wilaya wamtakiwa kuwa makini na viwanda vinavyokamua mbegu za alizeti kwa ajili ya mafuta kwa kuwa kuna maeneo wakulima wanaibiwa.