Katika kusaidia juhudi za maafa baada ya tetemeko kubwa la ardhi ambalo limesababisha vifo vya watu zaidi ya 3,000, na maelfu kadhaa kujeruhiwa, nchi ya Sudan imetuma timu ya watu 40 ya utafutaji na uokoaji nchini Uturuki.

Jeshi la Polisi nchini humo, kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani, timu ya wanachama wakiwemo wafanyakazi 7 wa Kikosi cha Ulinzi wa Wananchi waliondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Khartoum kueleke Gaziantep Ijumaa asubuhi ya Februari 10, 2023.

Baadhi ya waokoaji wanaojumuisha timu ya watu 40 kutoka nchini Sudan kuelekea nchini Uturuki. Picha ya Middle East Monitor.

Timu hiyo, ilibeba mablanketi 1000, mahema 250 na vifaa vya chakula pamoja na idadi kubwa ya vifaa vya utafutaji na uokoaji vitakavyosaidia shughuli za utafutaji na uokoaji chini ya uongozi wa mamlaka nchini Uturuki.

Mapema wiki hii, Algeria na Tunisia zilikuwa miongoni mwa nchi za kwanza barani Afrika kutuma msaada kwa nchi mbili za Uturuki na Syria.

Bodi DAWASA yaridhishwa maendeleo mradi JNHPP
Vyama haviwasaidii Wafanyakazi: CHADEMA