Kocha Mkuu mpya wa Tanzania Prisons, Fred Felix Minziro, ameanza kazi kwa kwa mara ya kwanza baada ya kuachana na Geita Gold akiomba ushirikiano kwa wachezaji na viongozi, na kufafanua kuwa hiyo ndiyo silaha kubwa ya ushindi, huku akiahidi kutengeneza timu itakayocheza soka safi la kuvutia, kasi na nguvu.

Minziro aliyechukua nafasi ya Mohamed Abdallah ‘Bares’, ambaye alitimkia Mashujaa FC, alisema anaamini Ligi Kuu msimu ujao itakuwa ngumu kuliko ya msimu uliomalizika, hivyo inabidi afanye kazi ya ziada kukiimarisha kikosi chake.

“Ligi inayokuja ni ngumu, lakini kikubwa ni kuwa mimi nimetoka Geita Gold na ilikuwa inafanya vizuri, kwa hiyo yalé yote niliyokuwa nayafanya nikiwa huko nayaleta hapa Prisons, kikubwa ni kupata ushirikiano kutoka kwa viongozi, wachezaji na mashabiki basi naamini Mungu ataleta heri zake,” amesema kocha huyo akiwa jijini Mbeya.

Minziro aliyechukua nafasi ya Mohamed Abdallah ‘Bares’, ambaye alitimkia Mashujaa FC, amesema kila mmoja anaelewa falsafa yake ya soka, na kwamba anataka kila anayekuja uwanjani kuiangalia timu yake awe ameridhika na kutojutia kiingilio chake alichotoa.

“Nataka kutengeneza timu ambayo kila mmoja akija kuiangalia ataridhika, icheze soka la kuvutia, kasi na nguvu, nataka aliyelipa kiingilio asijutie, anayetoka uwanjani timu ishinde, itoe sare au kufungwa aseme leo Prisons imepiga soka, hii ndiyo falsafa yangu,” amesema beki huyo wa zamani wa Young Africans na Taifa Stars miaka ya 1980.

Naye Nahodha wa timu hiyo, Jumanne El Fadhili, alisema watampa ushirikiano kocha huyo kama walivyofanya kwa walioondoka.

“Sisi tupo tayari kufanya kazi na kocha yeyote anayeletwa, kama wachezaji tumempokea na tutampa ushirikiano,” amesema nahodha huyo.

Ofisa Habari wa klabu hiyo, Jackson Mwafulango, alisema hii ni mara ya tatu kwa Minziro kuifundisha timu hiyo.

“Tumemrudisha kwa sababu tunaamini aina ya soka ambalo Prisons tunalitaka, tunamhitaji kocha huyu,” amesema Mwafulango.

Ibrahima Konate kujiongeza Liverpool
Hospitali ya Bombo kuwa kituo cha urekebishaji viungo