Karafuu hutumika kama kiungo na pia ni dawa muhimu kwa binadamu, ina uwezo wa kusaidia magonjwa mengi ikiwemo maradhi ya tumbo, meno na misuli vile vile hutumika katika kuleta harufu nzuri ya kinywa, mwili na mazingira ya nyumbani.
Fahamu faida za karafuu katika mwili wa bindamu
Unashauriwa, Ponda karafuu sita changanya na asali katika kijiko cha mezani kisha gawa mchanganyiko huo katika makundi mawili yanayolingana, ongeza chumvi kidogo katika kila moja pindi unapokuwa na kikohozi.
Lamba taratibu mchanganyiko huo kutwa mara mbili kama yalivyo makundi hayo kwa maana ya asubuhi moja na jioni, Endelea katika kipindi cha siku tatu hadi saba utaondokana na tatizo la kikohozi.
Wataalamu wanasema kuwa karafuu husaidia usagaji mzuri wa chakula tumboni na ni nzuri kwa matibabu ya maumivu ya tumbo, tumbo kujaa gesi na kiungulia. Hivyo, ni miongoni mwa kiungo muhimu katika vyakula kutokana na vinasaba vya aina ya eugnol vilivyomo ndani yake.
Matumizi ya karafuu na mafuta yake humfanya mtu kuwa mchangamfu humuondolea uchovu kwa vile karafuu inaiweka akili katika hali nzuri nakufanya ubongo ufanye kazi vizuri. Pia husadia kuondoa matatizo ya kusinzia, kupoteza kumbukumbu na wasiwasi.
Mafuta ya karafuu yanapochanganywa na chumvi, husaidia kuondosha maumivu ya kichwa, matatizo katika mfumo wa upumuaji, kusafisha koo na hutibu kikohozi, mafua na pumu.
Hata hivyo Karafuu hutumika kwenye vyakula mbalimbali ikiwamo nyama, biriani, pilau, mchuzi wa masalo na vyakula vikavu kama vile vileja, beskuti na donat na kwa upande wa vinywaji karafuu hutumika katika chai na maziwa.