Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharrif Hamad, ameeleza kuwa serikali inatarajia kuanzisha mfumo mpya wa ajira ikiwa ni hatua ya kuondoa ubaguzi wa ajira uliopo visiwani humo.
Seif ambae pia ni mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazelendo ameeleza hayo wakati wa ziara yake visiwani Pemba akikutana na viongozi mbalimbali wa serikali amnapo amekiri kuwepo kwa ubaguzi wa ajira kwa baadhi ya Wanzibari unaotokana na misingi ya tofauti za kisiasa.
“Kulikuwa na changamoto katika taasisi za kiserikali kuajiri, sasa serikali itaanzisha mfumo rasmi wa kimtandao kwa kuomba ajira na sio kama zamani”, amesema Maalim Seif.
Kwenye ziara hiyo pia Maalim Seif amesema, wanachi hususani vijana wanatarajiwa kunufaika na uwekezaji ambao uko njiani kufanyika katika sekta ya uvuvi.