Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amepanga mkakati mwingine wa kisiasa ambapo anatarajiwa kuanza kuwatembelea viongozi mbalimbali wastaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ili kukaribisha mazungumzo.

Imeelezwa kuwa Maalim Seif amemtumia ujumbe wa kutaka kukutana na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu CCM Visiwani Zanzibar, Ali Ameir kwaajili ya mazungumzo lakini juhudi zake ziligonga mwamba.

Aidha, kiongozi wa CUF aliyetumwa na Maalim Seif, ametajwa kwa jina moja la Kombo mkaazi wa Donge pangamaua mkoa wa Kaskazini Unguja.

“Nimefuatwa na mwanachama mmoja wa CUF aliyetumwa na Maalim Seif akitaka kuonana na mimi. sikuafiki jambo hilo kwa sababu sina ushuhuda wa ukuruba naye kisiasa au urafiki kindaki ndaki na mwanasiasa huyo.”amesema Ameir

 

Mpinzani wa Putin azuiliwa kugombea Urais
Eminem aukwapua mwaka 2017, avunja rekodi za Billboard