Mabehewa 14 ya Treni ya reli ya kisasa (SGR), yatakayotumika kusafirisha abiria nchini yamewasili toka Korea Kusini ikiwa ni miongoni mwa mabehewa 81 yanayohitajika ambapo 36 kati ya hayo tayari yamekamilika.
Tayari Mabehewa hayo 36 ambayo ni ya daraja la tatu yamesafaririshwa kuja nchini ambapo 45 yaliyobaki yanatarajiwa kukamilika mwezi Machi, 2023 na yatakuwa na huduma zote muhimu.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete amesema reli hiyo ya SGR kipande cha kwanza kilichojengwa toka Mkoani Dar es Salaam hadi Morogoro kinatarajiwa kuanza kutoa huduma zaake Januari, 2023.
Mapema mwezi Oktoba 2022, akiwa nchini Korea Kusini Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alitembelea kiwanda hicho cha Kampuni ya Sung Shin Rolling Stock kinachotengeneza mabehewa hayo ya reli ya kisasa (SGR).