Hatimaye Klabu ya Liverpool imekamilisha dili la pauni milioni 35 kumsajili kiungo kutoka nchini Argentina Alexis Mac Allister kutoka Brighton kwa mkataba wa miaka mitano.
Ada inaweza kupanda hadi pauni milioni 55 kwa kiungo huyo aliisaidia Brighton kumaliza nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England msimu huu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alifunga mabao 20 katika mechi 112 akiwa na Seagulls hao na kuisaidia Argentina kushinda Kombe la Dunia la 2022.
“Ni ndoto iliyotimia na siwezi kusubiri,” amesema Mac Allister.
“Nilitaka kuwa ndani kikosi cha Liverpool tangu siku ya kwanza ya maandalizi ya msimu mpya, kwa hiyo ni vizuri kwamba kila kitu kimekamilika. Ninatazamia kukutana na wachezaji wenzangu.”
“Ulikuwa mwaka mzuri kwangu Kombe la Dunia, kile tulichofanikiwa na Brighton lakini sasa ni wakati wa kufikiria juu ya Liverpool na kujaribu kuwa mchezaji bora na mwanadamu bora kila siku.”
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp anatazamia kuimarisha safu yake ya kiungo huku James Milner, Naby Keita na Alex Oxlade-Chamberlain wakiondoka Anfield msimu huu wa joto.
Walikuwa wamepunguzwa bei kutokana na uhamisho wa nyota wa Borussia Dortmund, Jude Bellingham, ambaye anaelekea kujiunga na Real Madrid baada ya klabu hizo kukubaliana ada ya euro 103.
Mac Allister alijiunga na Brighton kutoka Argentinos Juniors Januari 2019 na mara moja akarejea katika klabu hiyo ya jijini Buenos Aires kwa mkopo.
Ameichezea Argentina mara 16 na kuibuka kama mchezaji muhimu wakati wakitwaa taji lao la tatu la Kombe la Dunia Desemba.