Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali amekitosa chama cha NCCR- Mageuzi na kuhamia chama kipya cha ACT- Wazalendo.

Taarifa hizo zimetolewa rasmi na Naibu Katibu Mkuu wa ACT- Wazalendo, Msafiri Mtemelwa jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo pia alimtambulisha aliyekuwa Mwenyekiti wa Kitengo chaVijana wa NCCR- Mageuzi, Deo Meck.

Akithibitisha kujiunga na chama hicho kwa njia ya simu, Machali alisema kuwa anayo ‘yake ya moyoni’ ambayo amepanga kuyatoa Julai 21 katika mkutano utakaofanyika kwenye uwanja wa Kiganamo, Kasulu Mjini na kwamba atakuwa na Kiongozi Mkuu wa ACT- Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe.

Naibu Katibu Mkuu wa ACT- Wazalendo alieleza kuwa sio Machali pekee aliyehamia kwenye chama hicho bali kuna wabunge wengine wanne waliojiunga na chama hicho na wanatarajiwa kutambulishwa wakati wowote.

Makongoro Ajipanga Kumvaa Halima Mdee ‘Kawe’
Southampton Yampata Mrithi Wa Schneiderlin