Madaktari nchini Marekani wamepanga kufanya upasuaji na kupandikiza uume kwa mpiganaji wa zamani wa jeshi la nchi hiyo kwa lengo kumsadia kufanya ngono na kupata mtoto.

Upasuaji wa aina hiyo utafanyika kwa mara ya kwanza nchini humo na unatarajiwa kuchukua saa 12. Kwa mujibu wa madaktari, utahusisha ushonaji wa neva muhimu na mishipa ya damu kwa ajili ya kutunza mkojo ili kumsaidia mgonjwa huyo kushiriki tendo la ndoa.

Kwa mujibu wa CNN, Jopo la madaktari wa chuo kikuu cha John Hopkins (JHU) limepanga kufanya upasuaji huo kwa kuchukua uume kutoka kwa kijana mmoja ambaye ni marehemu aliyejitolea kutoa kiungo hicho kwa ruhusa ya familia yake.

Hata hivyo, madaktari hao wameeleza kuwa uwezo wa mgonjwa huyo mwenye umri wa miaka 60 kupata mtoto kutategemea jeraha na mafanikio ya upasuaji huo.

 

 

Video Mpya: Jux – One More Night
Balaa: Wanafunzi wa Vyuo Wasafiri Hadi Mlimani City 'Kutumia Vyoo Tu'!