Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Janeth Mayanja amesema mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia leo jumapili Novemba 3, Mkoani Manyara imesababisha mafuriko ya tope katika eneo la Katesh na Gendabi wilayani humo.
Amesema watu 20 wamefariki dunia na wengine takribani watu 70 wemejeruhiwa, mpaka kufikia mchana wa leo ambapo majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya wilaya Tumaini.
DC Mayanja amesema uokoaji unaendelea wa lutoa tope lilofunika nyumba, nyumba maduka na maeneo mbalimbali.
“Uokoaji unaendelea katika maeneo ya Katesh na Gendabi ambapo mafuriko hayo yamepita na kusomba nyumba kadhaa, maeneo ya biashara na kituo kikuu cha mabasi cha Katesh vfo mpaka sasa vimefikia 20” amesema DC Mayanja.