Rais Dkt. Joh Magufuli ameagiza vijana 800 wenye shahada waliojitolea katika jeshi la kujenga Taifa (JKT) kwa miaka 2 kuajiriwa serikalini kuanzia februari 2020.

Katibu mkuu ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa umma na utawala Bora, Dkt. Laureen Ndumbaro amesema kuwa Rais Magufuli aliagiza vijana hao waajiriwe kwa kuwa wamejitolea kwa muda mrefu hivyo wamejenga uzalendo.

Vijana hao wanatakiwa kuandika barua utumishi wakiambatanisha na nakala za vyeti vya taaluma pamoja na uthibitisho wa wakuu wa kambi zao na hapo watakuwa wamepata kazi.

Ikumbukwe kuwa katika kipindi cha 2019/2020 serikali imetangaza nafasi 40,000 za ajira ambazo zanaanza februali, lakini imeelezwa kuwa wataanza kuajiriwa vijana ambao hawazidi 800 wenye sifa.

Serikali yakemea uharibifu wa miundombinu kufanikisha biashara ya chuma chakavu
Watanzania wahimizwa usafi wa mazingira kipindi cha mvua