Rais Dkt. John Mgufuli ametoa tamko juu ya lawama zinanzoendelea nchini kuwa bei ya mahindi imepanda huku akiwataka wakulima waendelee kufurahia hali hiyo.

Magufuli akiwa Mkoani Morogoro leo Novemba 20 amesema, bei ya mahindi inapopanda na wengine wachache kulalamika ana uhakika wakati huo wakulima wanashangilia.

Amesema ” Nataka wakulima washangilie zaidi, na nataka kulisema hili kwa uwazi. ukiona mahindi yapo bei juu nenda kalime yako ya bei ya chini”

Na kusisitiza ” Biashara hii lazima iwe huru kwani mkulima anatafuta mbolea, anahangaika shambani akifukuzana na nyoka, matope ni yake, kuvuna ni yeye halafu umpangie bei? Bei itajipanga yenyewe”

Aidha ameongeza kuwa “Wakati wa kuwapangia bei wakulima umeshapita, katika kipindi changu sitapanga bei ya Mkulima na mimi ni mtoto wa mkulima ninafahamu maana ya kulima”

Live: Rais Magufuli akitatua kero za wananchi wa Chalinze mkoni Dodoma
JPM ampigia simu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA na kumpa maagizo mazito