Mahakama Kuu ya Tanzania imempa ushindi Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kufuatia rufaa aliyoikata akipinga hukumu dhidi yake iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Hai.

Mbowe alikata rufaa dhidi ya hukumu ya Mahakama ya hakimu Mkazi mjini Hai iliyoamuru afungwe jela mwaka mmoja au atoe faini ya zaidi ya shilingi 1,000,000 baada ya kumkuta na hatia katika kesi iliyokuwa ikimkabili ya kumshambulia msimamizi wa uchaguzi mwaka 2010.

Mahakama Kuu imeamua Mbowe arudishiwe kiasi cha shilingi 1,000,000 alizotoa kama faini katika mahakama ya mjini Hai.

Anna Mghwira Awataka Wananchi Kuzikataa Sinema Za CCM
Magufuli Awagusa Wafanyakazi Wa ‘Ndani’