Nyota kutoka wa muziki wa rap kutoka nchini Canada, Dizz Drake ameripotiwa kuruhusiwa kutofika mahakamani na kutotumia njia ya mtandao kutoa ushahidi kuhusu shutuma za kyhusishwa na tukio la mauaji ya rapa Xxxtentancion zilizotajwa kumkabili nyota huyo.

Kwa mujibu wa maelezo ya TMZ, inadaiwa kuwa pendekezo la rapa Drake limepokelewa na kukubaliwa na kwamba hautakuwapo utaratibu wa kuhojiwa na wakili wa utetezi juu ya shutuma hizo za mauaji.

Aidha hakimu Michael A. Usan amekubali kutia saini ombi la Dizz kutopanda kizimbani, huku akiiweka pembeni amri ya awali ya mahakama hiyo iliyomtaka Drake kufika mahakamani Februari 24 na 27 au kuwasilisha ushahidi wake kupitia njia ya mtandaoni.

Hiki ndio chanzo cha bifu la Rihanna na Trump

Hayo yalijiri siku kadhaa zilizopita baada ya wakili wa upande wa utetezi Mouricio Padilla kumtaja Drake kama mmoja wa wahusika wa kesi ya mauaji ya rapa Xxxtenticion kutokana na ugomvi uliokuwepo baina ya wasanii hao mapema mwaka 2017.

Licha ya shutuma hizo, hadi sasa rapa Drake hajazungumza chochote hadharani kuhusu kuhusishwa na mauaji hayo yaliyotokea Juni 18, 2018 Deerfield Beach Florida huko nchini Marekani.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Februari 16, 2023
Dkt. Tax na ujumbe wa Tanzania mkutano wa Mawaziri AU