Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewasili nchini Mauritius leo kwa ajili ya kumwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika mkutano wa kuzindua Jukwaa la Uchumi Barani Afrika (AEP).
Kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Sir Seewoosagur Ramgoolam Waziri Mkuu amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritius, Vishnu Lutchmeenaraidoo.
Uzinduzi wa jukwaa hilo unatarajiwa kufanyika kesho mjini Port Louis ambapo utawakutanisha viongozi wakuu wa nchi za Afrika, wanazuoni, wafanyabiashara pamoja na watu kutoka kwenye asasi mbalimbali za kiraia barani Afrika.
Aidha, Waziri Mkuu mara baada ya kumaliza mkutano huo anatarajia kutembelea maeneo maalumu ya uwekezaji, viwanda vya sukari na nguo.
Hata hivyo, Waziri Mkuu ameambatana na Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Dkt. Khalid Salum Mohammed na Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage pamoja na maofisa wengine wa Serikali.