Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa serikali haijaupa kipaumbele mchakato wa Katiba mpya, bali inataka kwanza kuhakikisha Watanzania wanapata huduma za Kjamii kama, elimu, maji, afya na miundombinu.

Ameyasema bungeni mjini Dodoma wakati wa masawali na majibu, baada ya kuulizwa swali na mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea (CUF) aliyetaka kujua lini serikali itakamilisha mchakato huo.

Amesema kuwa suala la Katiba si miongoni mwa vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Tano kwani kukamilisha mchakato huo kunahitaji fedha nyingi na gharama kubwa ambapo kwa sasa fedha zinazo kusanywa zinaelekezwa katika kuboresha huduma za jamii.

“Mchakato wa Katiba ni gharama na Serikali inatambua umuhimu wake, hivyo kwa sasa inalenga kuboresha huduma kwa wananchi kwa kutumia Katiba iliyopo,”amesema Majaliwa

Hata hivyo, ameongeza kuwa mchakato wa Katiba unalenga kufanya marekebisho ya mambo mbalimbali ambayo yamo katika Katiba ya sasa, hivyo iliyopo itaendelea kutumika hadi hapo fedha zitakapopatikana.

 

Polisi: Mnunuzi wa nyumba za Lugumi alitumwa na Lugumi
LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Novemba 10, 2017