Aliyekuwa  Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA), Dkt. Willbrod Slaa ameajiriwa katika duka moja kubwa linalouza bidhaa za majumbani (Supermarket) la Cosatco lililoko Oakville, Toronto nchini Canada.

Dkt. Slaa ambaye pia aliwahi kuwa mbunge wa Karatu kwa vipindi vitatu kwa sasa anaishi nchini Canada, ambako alikwenda kwa masomo tangu alivyotangaza kuachana na siasa, mwaka 2015.

Aidha, katika mitandao ya kijamii hivi karibuni kumezuka taarifa kuwa katibu huyo za zamani wa Chadema amemaliza masomo yake na sasa anafanyakazi katika moja ya maduka makubwa nchini humo (Supermarket), akihudumia kama mshauri wa mauzo akilipwa Dola za Marekani 10 (zaidi ya sh. 20,000) kwa saa.

“Niko ninafuatilia ziara ya Rais Dkt. Magufuli kule Mutukula, nimesema siku zote ninaishi kwa jasho na kazi ya mikono yangu, Canada ili uishi vizuri ni lazima ufanye kazi zaidi ya mbili au tatu mpaka nne, hayo nimeweka wazi sijui kama kuna mtu hafuatilii hili,”amesema Dkt. Slaa

Hata hivyo, ameongeza kuwa kila mara amekuwa akiwataka vijana wa Kitanzania kufanya kazi kwa bidii kwani fedha haziji kwa kukesha kwenye mitandao na kupiga soga vijiweni.

Papa Francis apiga marufuku uvutaji wa sigara Vatican
Polisi: Mnunuzi wa nyumba za Lugumi alitumwa na Lugumi