Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ameziagiza mamlaka husika kuchukua hatua kali za kisheria kwa watakaobainika kuwanyanyapaa na kuwabagua Watu Wanaoishi na Virusi vya ukimwi (WAVIU) kwani vitendo, kauli au mitazamo ya unyanyapaa na ubaguzi kwa kundi hilo havikubaliki.

“Kumekuwa na madai kuwa watumishi wa afya wana tabia za unyanyapaa na kuvujisha siri za WAVIU wanapotoa huduma katika vituo vyetu vya tiba na matunzo kwa WAVIU, Vitendo na tabia hizi ziripotiwe mara moja pindi vitakapotokea,” Amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Ametoa agizo hilo leo Desemba Mosi, 2021 alipomuwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani yenye kauli mbiu ya zingatia usawa tokomeza ukimwi tokomeza magojnwa ya mlipuko ambapo maadhimisho kitaifa yamefanyika mkoani Mbeya

Ameongeza kuwa vitendo vya unyanyapaa kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi vinakwaza na kurudisha nyuma mapambano dhidi ya Ukimwi nchini, kwa kuwa baadhi ya watu wanaoishi na VVU wanashindwa kutojitokeza na kupata huduma.
 
Kwa mujibu wa Waziri Mkuu Majaliwa, katika kudhibiti kuenea kwa maambukizi mapya ya Ukimwi Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo inaendelea kutekeleza mkakati wa nne wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi kwa kushirikisha sekta zote nchini.
 
 
Amesema mkakati huo wa mwaka 2018/2019 hadi 2022/2023 umelenga kupunguza maambukizi mapya ya virusi vinavyosababisha ukimwi pamoja na vifo.
 
 

Bahanuzi: Wachezaji Simba SC wana bahati
Nilikubali kuolewa Ili kuokoa familia yangu